DETROIT: Serikali ya Bush iache kutega mazungumzo ya simu
18 Agosti 2006Matangazo
Juhudi za rais wa Marekani,George W.Bush kutega mazungumzo ya simu nchini humo,kama sehemu ya vita dhidi ya ugaidi,zimepata pigo baada ya jaji mkuu kuiamuru serikali yake isitishe mpango wa kutega simu.Jaji amesema,kusikiliza maongezi ya watu kwa siri na kudaka barua pepe bila ya idhini,huenda kinyume na katiba na hukiuka sheria za faragha.Serikali ya Bush imetetea mpango wake kama ni chombo kinachohitajiwa katika vita vyake dhidi ya ugaidi.