1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

DHAKA: Watu takriban 50 wajeruhiwa katika machafuko

8 Januari 2007

Watu wasiopungua 50 wamejeruhiwa leo mjini Dhaka kufuatia machafuko baina ya polisi wa kuzuia fujo na waandamanaji wanaotetea mageuzi. Watu 30 wametiwa mbaroni na wanazuiliwa na polisi.

Polisi walilazimika kutumia gesi ya kutoa machozi na risasi za mpira kuwatawanya waandamanaji waliokuwa wakilenga kwa mawe mjini humo. Watetezi mageuzi wameendeleza mgomo wa usafiri uliokwamisha shughuli zote mjini Dhaka.

Waandamanaji wanataka mageuzi ya sheria za uchaguzi yafanywe na uchaguzi uliopangwa kufanyika tarehe 22 mwezi huu uahirishwe.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW