1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
UchumiKenya

Dhuluma dhidi ya watoto zaongozeka Busia

18 Julai 2024

Visa vya watoto kudhulumiwa vimeongezeka kwenye jimbo la mpakani mwa Kenya na Uganda la Busia. Watoto wanajihusisha na shughuli za biashara badala ya kwenda shule.

Watoto nchini Kenya
Wanafunzi wanaoishi kwenye makazi yasiyo rasmi wakiwa wanatizama utengenezaji wa mchezo unaochezwa wakati wa Christmas Picha: Luis Tato/AFP

Katika maeneo ya barabarani utaona vijana wadogo wanafanya biashara za uchuuzi wa bidhaa mbali mbali hadi migodini.

Soma pia:Nusu ya Wakenya wako kwenye mkwamo wa kifedha - Utafiti

Na kwenye ziwa Viktoria utawaona vijana wakifanya uvuvi wa samaki. Hizi ni miongoni mwa ajira kwa watoto, katika jimbo la Busia ambako viwango vya umaskini vinahusishwa na ongezeko la ajira miongoni mwa watoto.

Kando na umaskini, utafiti ulioendeshwa na shirika la nchini Uholanzi la Terre Des Hommes unaonyesha kuwa, jimbo la Busia linaongoza kwa ajira za watoto ikizingatiwa uwepo wake mpakani mwa Kenya na Uganda, lakini pia dhuluma za kimapenzi na ulanguzi wa binadamu.

Soma pia: Umoja wa Mataifa wachunguza utumwa wa ngono Sudan

Watu nchini Kenya wakiwa wameandamana kupinga utendaji wa serikali ambao wanasema umesababisha umasikini kwa wananchi wengiPicha: Thomas Mukoya/REUTERS

Utafiti huo unaonesha kwamba asilimia 45 ya watoto wanaoenda shule wameajiriwa na hata asilimia 55 ya ambao hawaendi shule pia wakiwa wameajiriwa. 

Lawama nyingi zimeelekezwa kwa wazazi na walezi kutokana na kuongezeka kwa vitendo hivyo, kutokana na kushindwa kuwajibika ipasavyo kukidhi mahitaji ya msingi.

Wakati takwimu hizi zikiongezeka, serikali ya Kenya imekwishaahidi kuimarisha juhudi za kupambana na visa vya ajira miongoni mwa watoto na kusisitiza watoto kupelekwa shuleni.

Kwa mujibu wa takwimu za shirika la kimataifa la kuwahudumia watoto UNICEF mwaka 2023, watoto wa umri kati ya 5 hadi 17 walihusishwa katika ajira za watoto ambazo zilikuwa hatari kwa afya na ukuaji wao.

Sikiliza: 

Kadhia ya dhuluma dhidi ya watoto Kenya

This browser does not support the audio element.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW