1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Die Linke chatangaza wagombe uchaguzi wa mapema Ujerumani

Angela Mdungu
10 Novemba 2024

Chama cha mrengo wa kushoto cha Die Linke nchini Ujerumani kimetangaza Jumapili kuwa kimewachagua wagombea wake watakaoshiriki kwenye uchaguzi wa mapema unaotarajiwa kufanyika mwakani.

Die Linke chatangaza wagombea wake
Heidi Reichinek na Jan van Aken watapeperusha bendera ya chama cha Die Linke katika uchaguzi wa mapema wa Ujerumani mwakaniPicha: Fabian Sommer/dpa/picture alliance

 Mwenyekiti mwenza wa chama hicho Jan van Aken na mbunge Heidi Reichinnek ndiyo watakiongoza kwenye kiny'anganyiro hicho.

Soma zaidi:Uchaguzi wa Ujerumani unafanyikaje? 

Akizungumza katika mkutano na vyombo vya habari kiongozi mwenza Ines Schwerdtne amesema wanaingia kwenye kampeni za uchaguzi wakiwa kitu kimoja akiashiria kuwa wagombea wamepitishwa kwa sauti moja.

Chama hicho cha mrengo wa kushoto, kimeporomoka katika uungwaji mkono tangu mmoja wa viongozi wake wa ngazi ya juu Sahra Wagenknecht alipojiondoa na kuanzisha chama chake kilichobeba jina lake. Kwa sasa bado haifahamiki ikiwa Die Linke kitavuka kihunzi cha kupata asilimia 5 inayohitajika kuingia bungeni.