1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Diego Costa aendelea kuwika Uingereza

Admin.WagnerD30 Septemba 2014

Diego Costa alipachika goli lake la nane katika ligi ya Uingereza , Premier League wakati viongozi Chelsea wakiendelea na mwanzo mzuri kwa kupata ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Aston Villa.

Fußball Chelsea Diego Costa
Picha: Reuter/Toby Melville

Edin Dzeko aliufumania mlango mara mbili wakati mabingwa Manchester City ikipata ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya Hull City na kuchupa hadi nafasi ya tatu katika msimamo wa ligi , point mbili nyuma ya Southmpton , iliyoishinda Queens Park Rangers kwa mabao 2-1.

Manchester United imesogea katika nafasi ya saba ikiwa imepata ushindi wake wa pili msimu huu chini ya kocha Luis van Gaal kwa ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya West Ham United.

Arsenal na Tottenham Hotspurs , Liverpool na Everton ziliridhika na sare wakati mapambano ya watani wa jadi mjini London yakiishia kwa sare ya bao 1-1.

Nchini Uhispania , Barcelona na Real Madrid zimeendelea kufukuzana wakati timu zote hizo zikipata ushindi mwishoni mwa juma, ambapo Atletico Madrid haikuachwa nyuma ambapo iliiadhibu Seville kwa kuitwanga mabao 4-0.

Mwandishi: Sekione Kitojo / afpe / dpae / rtre , ZR
Mhariri: Iddi Ssessanga

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW