SiasaDjibouti
Djibouti kufanya uchaguzi wa rais siku ya Ijumaa
10 Aprili 2026
Matangazo
Rais wa Djibouti, Ismail Omar Guelleh, anatafuta nafasi ya kuiongoza nchi hiyo ya Pembe ya Afrika kwa muhula wa sita na atachuana na mgombea mmoja tu asiye na umaarufu sana Mohamed Farah Samatar, ambaye ni kiongozi wa Chama cha Unified Democratic Center (CDU), ambacho hakina hata kiti kimoja bungeni.
Zaidi ya wapiga kura 256,000 wanatarajiwa kushiriki uchaguzi huo. Guelleh ameiongoza nchi hiyo yenye takriban wakaazi milioni moja kwa mkono wa chuma kwa miaka 27. Nchi hiyo ndogo inahifadhi kambi na vikosi vya kijeshi kutoka Ufaransa, Marekani, China, Japan na Italia, jambo linalozalisha faida kubwa za kifedha, kiusalama na kisiasa.