Djokovic apewa taji baada ya Federer kujiondoa
17 Novemba 2014Matangazo
Mswisi huyo mwenye umri wa miaka 33, ambaye alimbwaga mwenzake Stanislas Wawrinka katika nusu fainali usiku uliotangulia, alitangaza uamuzi huo katika uwanja wa O2 Arena uliokuwa umerufika kwa ajili ya fainali hiyo.
Hivyo basi Djokovic anayeorodheshwa nambari moja ulimwenguni katika mchezo wa tennis kwa wanaume, ndiye mchezaji wa kwanza wa Tennis kushinda Finali hizo za ATP World Tour kwa miaka mitatu mfululizo lakini hakuonekana kuwa mwenye furaha wakati akipokea kombe pamoja na hundi ya dola milioni 1.92… labda kwa sababu hakuutolea jashi ushindi huo…
Mwandishi: Bruce Amani/AFP/Rueters
Mhariri: Yusuf Saumu