1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

CHADEMA yampoteza Slaa

Hawa Bihoga25 Septemba 2015

Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Wilbroad Slaa, amejitokeza hadharani kwa mara ya kwanza baada ya kimya cha muda mrefu na kutangaza kujitoa kwenye chama chake.

Aliyekuwa Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Wilbroad Slaa.
Aliyekuwa Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Wilbroad Slaa.Picha: DW/M.Khelef

Dk. Slaa alisema hawezi kumuunga mkono mgombea urais wa chama hicho anayeuwakilisha Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA), Edward Lowassa, akidai kuwa mgombea huyo anahusika katika kashfa za kuhujumu fedha za umma ikiwemo ile ya Richmond. Msikilize mwaandishi wetu Hawa Bihoga akiwa Dar es Salaam na ambaye alihudhuria mkutano huo wa Dk. Slaa na waandishi wa habari.

Mwandishi: Hawa Bihoga//DW Dar es Salaam
Mhariri: Mohamed Abdul-Rahman

Ruka sehemu inayofuata Gundua zaidi

Gundua zaidi

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW