1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Dkt. Edward Hosea ndio Rais wa TLS Tanzania

16 Aprili 2021

Chama cha wanasheria Tanganyika TLS, kimemchagua Dr. Edward Hosea kuwa Rais wa chama hicho katika uchaguzi uliofanyika jijini Arusha. Hosea aliwahi kuwa kiongozi wa taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa Takukuru

Tanzania, Arusha | Tanganyika Law Society TLS
Picha: Veronica Natalis/DW

Mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi Charles Rwechungura amemtangaza Dkt. Hosea kuwa mshindi kwa kura 297 na kuwashinda wenzake wanne aliokuwa akichuana nao katika kiti nafasi hiyo ya juu kabisa ya uongozi katika chama hicho kinachosimamia misingi ya haki na sheria.

"Dkt. Edward Hosea amepata kura 297, kwahiyo naona hamukushangilia sana kwasababu mmeshajua haya mambo, tumepata fununu kuna mtu alitusaliti lakini sisi tumesema tulichonacho ndio hicho," alisema Rwechungura alipokuwa anamtangaza Dkt Hosea kuwa rais wa TLS

Mwaka 2008 Dr. Hosea alikuwa kiongozi mkuu wa taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa Takukuru, ambapo hata hivyo wakati anaachia kiti hicho, taasisi hiyo ilikumbwa na kashfa ya rushwa ya mradi wa nishati ya umeme Richmondi, ambayo ilisababisha waziri mkuu wa Tanzania wa kipindi hicho Edward Lowasa kujiuzulu.

Hosea asema ataendelea kusimamia misingi ya haki na sheria

Wajumbe wa chama cha wanasheria Tanganyika TLS katika mkutano wa chama uliofanyika mjini Arusha Picha: Veronica Natalis/DW

Dr. Hosea naye aliondoka katika nafasi yake lakini mara kadhaa amekuwa akikanusha kuhusika na madai hayo. Lakini yeye mwenye baada ya kutangazwa kuwa mshindi wa kiti cha urais wa TLS anasema ataendelea kusimamia misingi ya haki na sheria.

soma zaidi: Fatma Karume asema TLS si mali ya umma

Kalebu Lameck Gamaya wakili na mpig akura, anasema kuwa anaimani uongozi huu mpya utaendeleza yale mazuri yaliyofanywa na uongozi uliopita, huku akitoa wito wa kusimamiwa kwa misingi ya haki na utawala wa kisheria, kujali maslahi ya mawakili na kupinga sheria zote kandamizi.

Nafasi ya urais wa chama hicho ilikuwa ikigombaniwa na mawakili watano ambao ni Albert Msando wakili maarufu nchini Tanzania, Shehzad Wall, Rais wa zamani wa chama hicho Francis Stolla, na mwanamke pekee Flaviana Charles.

Mwandishi: Veronica Natalis DW Arusha.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW