1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

DNC: Kamala Harris aihimiza Marekani kuchukua mwelekeo mpya

23 Agosti 2024

Makamu wa Rais Kamala Harris amewataka Wamarekani kukataa migawanyiko ya kisiasa na badala yake kuchora kile alichokiita njia mpya ya kusonga mbele katika hotuba ya kukubali uteuzi wa chama chake kugombea urais.

Marekani Chicago | Mgombea wa  Kamala Harris
Mgombea wa urais nchini Msrekani Kamala Harris, akitoa hotuba ya kukubali kuwa mgombea wa urais kupitia chama cha DemocratPicha: J. Scott Applewhite/dpa/AP/icture alliance

Maputo yaliteremka kwenye uwanja wa United Arena, wakati Makamu wa Rais Kamala Harris alipokubali rasmi uteuzi chama cha Democratic kuwa mgombea wake wa urais, na kuhitimisha wiki nne za harakati tangu wakati mgombea wa awali, Rais Joe Biden, alipojiondoa katika kinyang'anyiro hicho.

Mkutano huo Mkuu wa Democratic ulikuwa kwa sehemu, tukio la kutoa heshima kwa Biden, ambaye utumishi wake wa miongo mitano ulifikia kilele cha urais.

Lakini zaidi ulikuwa jukwaa la uzinduzi wa tiketi ya Harris-Walz, kufuatia uidhinishaji wa wanachama mashuhuri, wakiwemo viongozi wa zamani na wa sasa, na nyota wa muziki na utamaduni kama vile Oprah Winfrey na Stevie Wonder.

Soma zaidi: Kamala akubali rasmi uteuzi wa kugombea urais Marekani

Baada ya siku kadhaa za kuwa na watu kama akina Obama, Clinton, mume wa Harris, Doug Emhoff na Spika wa zamani Nancy Pelosi waliotoa hotuba za kumuunga mkono, hatimaye wakati ulifika kwa Harris kujinadi.

Alitoa ujumbe uliopambwa kwa maono ya matumaini, kusonfa mbele, na uliojaa ahadi za kutetea uhuru wa uzazi na kujenga uchumi wa fursa.

"Najua kuna watu wenye mitazamo mbalimbali ya kisiasa wanaotazama usiku wa leo. Na nataka mjue, ninaahidi kuwa rais wa Wamarekani wote. Mnaweza kuniamini wakati wote kutanguliza maslahi ya nchi juu ya chama na mwenyewe," alisemaHarris.

Na kulikuwepo na mengi ya kuashiria kwamba hadhira ilipokea ujumbe wake.

Maadili ya Marekani yachukuwa nafasi kuu

"Nadhani kurudisha kwake maadili ya Marekani, wito kwa watu wote ambao wanaweza kujivunia nchi yetu kwenye uwanja wa kitaifa, uwanja wa ndani, vipaumbele vyote vya sera vinavyowaweka mahali pazuri Wademokrat, sio kwa Wamarekani tu, bali kwa watu wa asili na asili zote, hilo ni jambo ambalo ninalifurahia sana,” alisema Cameron Deptula, mjumbe kutoka Hawaii.

Mgombea wa urais nchini Marekani Kamala Harris awataka Wamarekani kuepuka migawanyikoPicha: J. Scott Applewhite/dpa/AP/picture alliance

Matt Golosinski, mkurugenzi wa Mawasiliano ya Utafiti katika Chuo Kikuu cha Northwestern, alisema ujumbe kuhusu Wamarekani wote kuungana pamoja ulikuwa wa kuvutia sana.

"Jambo kuu lilikuwa wazo hili la kila mtu kufanya kazi pamoja, kuinua kila mtu, badala ya kuwatenganisha watu. Huo ni ujumbe muhimu sana kwa kila mahali duniani. Ni rahisi kusema kuliko kufanya, lakini nadhani tunaweza kuanzia nyumbani," aliiambia DW.

Maadili ya kijamii na umuhimu wa kusaidia wengine yalikuwa mada inayojirudia katika kongamano hilo, ambalo makamu wa rais Tim Walz aliizungumzia sana alipokuwa akitoa hotuba yake mwenyewe - akiangazia historia yake kama mwalimu wa shule ya umma na mkufunzi wa mpira wa miguu, huku akilaani kile alichokosoa kama ajenda ya kujitegemea ya mgombea wa Republican Donald Trump.

"Tulihakikisha kwamba kila mtoto katika jimbo letu anapata kifungua kinywa na chakula cha mchana kila siku," alisema, akimaanisha mswada wa jumla wa chakula cha mchana shuleni bila malipo aliotia saini kuwa sheria katika jimbo lake la Minnesota. "Wakati majimbo mengine yalikuwa yakipiga marufuku vitabu kutoka kwa shule zao, tulikuwa tukiondoa njaa ya watoto kutoka kwetu."

Joe Barbuto, mwenyekiti wa chama cha Democrats Wyoming, aliiambia DW kwamba aliona chaguo la Walz kama mgombea mwenza kama ishara ya hamu ya Harris kufikia kitovu.

"Hakika yeye ni mtu ambaye ana asili dhabiti katika Amerika ya vijijini na amefanya mawasiliano mengi katika Amerika ya vijijini, kama mbunge, kama gavana," alisema Barbuto. "Hilo linapaswa kuwa jambo la kutuambia kwamba ana nia ya kuzingatia sio tu majimbo ya bluu, lakini taifa letu."

Sifa za sera za kigeni za Harris chini ya uchunguzi

Lakini kwa baadhi ya waliohudhuria, kulikuwa na wasiwasi kuhusu msimamo wa sera ya kigeni wa Harris ambao ulikuwa umeenea. Hii ilidhihirika hasa kwa wajumbe wanaowakilisha zaidi ya wapiga kura 700,000 ambao walipiga kura zao "kutojifunga" katika mchujo wa Democratic kushinikiza utawala wa Biden-Harris kukomesha uungaji mkono wa kisiasa na kijeshi kwa Israeli kuhusiana na vita vyake dhidi ya Hamas huko Gaza.

"Kama mjumbe asiejifunga, tunamtaka Harris kushinikiza usitishaji vita wa kudumu na wa mara moja na marufuku ya silaha sasa hivi, na bila shaka tunatambua ukweli kwamba hilo lilitajwa, lakini kwa nukta hii maneno hayatoshi, ahadi tupu hazitoshi, tunahitaji kujua sera zake ni zipi," alisema Sabrene Odeh, mjumbe asijefunga kutoka jimbo la Washington, kufuatia hotuba ya Harris.

Je, Harris na Walz watabakia na matumaini yaliyopo sasa?

Kamala Harris, anayewania urais nchini Marekani akiwa na mgombea mwenza Tim WalzPicha: Anna Moneymaker/Getty Images

Vita hivyo vinasalia kuwa moja ya masuala yanayosababisha mgawanyiko katika chama ambacho kilifanya haraka kuonyesha umoja katika kumuunga mkono Harris. Na nje ya DNV, maelfu ya waandamanaji wanaowaunga mkono Wapalestina walilenga kufahamu kinachoendelea ndani ya mkutano huo - ingawa wengi wao walisema hakuna kitu ambacho Wademokrat wangefanya kupata kura zao.

Soma pia:Walz ahutubia mkutano mkuu wa chama cha Democratic Marekani

"Muungano wetu ni mpana, na tuko kote nchini, hivyo ni vigumu kusema ni jinsi gani kila mtu anavyohisi," mratibu wa maandamano Faayani Aboma Mijana alisema. "Lakini naweza kuzungumza na shirika langu. Naweza kuzungumza na mtandao wa jumuiya ya Wapalestina wa Marekani. Hatupigi kura kwa wakati huu, ukweli kwamba Kamala Harris na Donald Trump wako mezani, tunaona kama dalili ya mfumo mbovu. Mfumo huu unahudumia matajiri na wenye nguvu pekee, na kwa kufanya hivyo, unatupa chaguzi hizi mbili tu, na zote mbili kwa wakati huu ni mbaya sawa."

Licha ya wasiwasi wa waandamanaji, DNC ilikuwa ni tukio la siku nne la sherehe na msisimko kuhusu tiketi mpya rasmi ya Demokratic. Lakini zikiwa zimesalia zaidi ya siku 70 hadi uchaguzi ufanyike, swali linabakia kama Harris na Walz wataweza kuwa na hali hiyo ya matumaini hadi kufikia ushindi wa uchaguzi.

Wademokrati waliokusanyika kwenye mkutano huo wa taifa walitabiri kwamba Kamala Harris atamshinda Donald Trump. Lakini mtihani wa kweli kwa Harris ndio umeanza. Mgombea huyo bado hajaanza kuelezea mipango ya kina ya sera.

Bado hajakaa chini kwa mahojiano hata moja ya kina ya vyombo vya habari ili kukabiliana na maswali magumu kuhusu mabadiliko yake ya kisiasa. Na anasalia kutoeleweka kwa sehemu kubwa kwenye akili za wapigakura wengi.

Sikiliza Mjadala:

MMT FE: Maoni - Trump vs Kamala for US President ? 24/25.08.2024 - MP3-Stereo

This browser does not support the audio element.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW