DOHA:Zawahiri asema al-Qaeda itaendelea kulenga mashambulio yake dhidi ya Marekani na washirika wake
21 Desemba 2006Matangazo
Kiongozi nambari mbili wa mtandao wa kigaidi wa Alqaeda Ayman-Zawahiri amesema kundi hilo litaendelea kuilenga Marekani pamoja na nchi nyingine za Magharibi hadi pale mashambulizi dhidi ya waislamu yatakapokomeshwa.
Katika ukanda wa video uliorushwa hewani na kituo cha televisheni cha kiarabu cha Aljazeera Zawahiri pia amepinga hatua ya rais Mahmoud Abbas ya kutaka ufanyike uchaguzi wa mapema nchini Palestina.
Badala yake al Zawahiri amewaambia wapalestina kitakachowakomboa ni vita takatifu vya Jihad pekee.