Dola 900,000 za misada zaibiwa huko nchini Kongo
7 Juni 2023Matangazo
Shirika hilo limesema katika taarifa yake kwamba wizi huo ulifanywa na wafanyakazi wa ndani wa shirika hilo kwa kushirikiana na watu wa nje.
Zaidi ya familia 1,700 maskini ambazo zilihitaji misaada zimeathirika na wizi huo uliotendeka kwa kipindi cha zaidi ya miezi sita kuanzia mwezi Agosti mwaka 2022.
Uchunguzi unafanyika ili angalau kurejesha sehemu ya fedha hizo ingawa kiasi kikubwa cha pesa hiyo huenda kisipatikane.
Shirika la GiveDirectly hutoa misaada kupitia teknolojia ya miamala ya kwenye simu, ambayo linasema kuwa inaepuka aina nyingi za wizi.
Eneo la mashariki mwa Kongo ambako shirika hilo linafanya kazi, limekumbwa na mzozo kwa miongo kadhaa.