1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

Donald Trump aanza kupanga safu yake ya wasaidizi

8 Novemba 2024

Rais Mteule wa Marekani Donald Trump amefanya uteuzi wa kwanza wa wasaidizi wake wakati anajitayarisha kuchukua madaraka mnamo Januari mwaka ujao baada ya kushinda uchaguzi uliofanyika siku ya Jumanne.

Uchaguzi 2024 Trump | Susie Wiles
Susie WilesPicha: Alex Brandon/AP Photo/picture alliance

Trump amemteua meneja wake wa kampeni Susie Wiles kuwa mkuu wa utumishi wa ikulu ya White House; wadhifa wenye jukumu la kusimamia shughuli za kila siku za ofisi ya rais na watumishi wake.

Kwenye taarifa yake, Trump amesema Susie amemsadia kupata ushindi wa kishindo katika uchaguzi uliomalizika na alikuwa na mchango mkubwa kwenye kampeni yake ya mwaka 2016 na 2020. Trump amemwelezea Susie kuwa kiongozi madhubiti, mwenye maarifa na mbunifu.

Katika hatua nyingine Rais Vladimir Putin wa Urusi amempongeza Trump kwa ushindi aloupata na kuashiria yuko tayari kufanya naye mazungumzo.

Salamu kama hizo zimetolewa pia na Rais Xi Jinping wa China aliyemsihi Trump kufanya kazi kwa dhamira ya kuzipatanisha nchi hizo mbili zenye mahusiano yaliyodorora.