1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUingereza

Donald Trump afanya ziara rasmi Uingereza

16 Septemba 2025

Rais wa Marekani Donald Trump amewasili Uingereza kwa ziara rasmi ya siku mbili ambapo serikali ya Uingereza inatumai kusaini mkataba wa kiteknolojia wenye thamani ya mabilioni ya dola.

Washington D.C. Marekani, 2025 | Keir Starmer na Donald Trump
Rais Trump wa Marekani na mwenyeji wake Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Starmer watarajiwa kusaini mikataba ya kibiashara na kiteknolojia mjini London.Picha: Carl Court/empics/picture alliance

Mkataba huo utaonesha kuwa ushirikiano wa Marekani na Uingereza unasalia kuwa imara licha ya tofauti kuhusu mizozo ya Ukraine, Mashariki ya kati na pia kuhusu mustakabali wa miungano ya nchi za Magharibi.

Trump kwanza atakutana na Mfalme Charles III katika kasri lake Windsor, kisha baadaye atakutana na Waziri Mkuu Keir Starmer.

Miongoni mwa mikataba inayotarajiwa kusainiwa wakati wa ziara ya Trump ni pamoja na utakaoharakisha miradi mipya ya nyuklia na kile maafisa wa Uingereza wamekiita "ushirikiano wa kiteknolojia wa hali ya juu duniani".

Kabla ya ziara hii, kampuni ya Google ilitangaza kuwa itawekeza pauni bilioni 5 nchini Uingereza katika kipindi cha miaka miwili ijayo.

Nayo kampuni za kifedha za Marekani kama PayPal na Citi Group zilitangaza uwekezaji wa pauni bilioni 1.25.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW