Donald Trump kuapishwa kuwa rais wa 47 wa Marekani
20 Januari 2025Hii itakuwa ni mara ya pili kwa Trump kurejea katika Ikulu ya Marekani kwa kipindi cha miaka minne baada ya kushinda katika uchaguzi mkuu wa mwezi Novemba mwaka uliopita.
Trump atachukua nafasi ya rais Joe Biden anayeondoka Ikulu hii leo ikiwa ni miezi miwili na nusu baada ya kumshinda Makamu wa Rais anayemaliza muda wake Kamala Harris katika uchaguzi mkuu.
Majira ya asubuhi kwa saa za Marekani, Trump atahudhuria ibada katika kanisa la Mtakatifu Johns mjini Washington. Baada ya hapo itafuata sherehe ya kuapishwa kwake na kisha Biden atampokea Trump Ikulu kwa dhifa ya chai.
Awali sherehe ya uapisho ilipangwa kufanyika katika eneo la siku zote nje ya Bunge la Marekani lakini zimehamishiwa ndani kwa sababu ya hali ya hewa katika jiji la Washington. Baada ya kuapishwa Trump atatoa hotuba yake yake ya kwanza kama rais wa 47 wa Marekani.