1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

Donald Trump anusurika jaribio la pili la kuuawa

16 Septemba 2024

Mgombea urais wa chama cha Republican nchini Marekani,Donald Trump, yuko salama baada ya hapo jana maafisa wa upelelezi, kuzima kile walichosema lilikuwa jaribio la kumuuwa.

Uchaguzi Marekani 2024| Donald Trump
Jaribio la mauaji dhidi ya Trump ni la pili katika kipindi cha miezi miwili.Picha: Win McNamee/UPI Photo via Newscom picture alliance

Maafisa wengi wa shirika la upelelezi la Marekani,FBI walimfyetulia risasi mtu mmoja aliyekuwa na bunduki katika eneo la kichaka,karibu na eneo la uwanja wa mchezo wa mpira wa Golf,alikokuwa anacheza Trump huko Florida.

Mshukiwa huyo alifanikiwa kukimbia na kuacha bunduki yake aina ya Ak-47 na vitu vingine lakini baadae akakamatwa.

Vyombo kadhaa vya habari nchini Marekani, ikiwemo CNN vimeripoti kwamba mshukiwa wa jaribio hilo ni mwanamme kwa jina Ryan Wesley Routh, mwenye umri wa miaka 58, kutoka Hawaii.

Jaribio hilo la mauaji dhidi ya Trump ni la pili katika kipindi cha miezi miwili.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW