Donald Trump ashinda uchaguzi wa Rais wa Marekani
9 Novemba 2016Matangazo
Wamarekani wamemchagua Donald Trump kuwa rais wa 45 wa nchi hiyo. Amejikingia sauti 276 dhidi ya 218 za wawakilishi wa majimbo. Rais mteule Trump amewahutubia wafuasi wa chama chake na wamarekani kwa jumla. Mgombea wa chama cha Democrats Hillary Clinton ameungama ameshindwa na ameshazungumza kwa simu na Donald Trump kumpongeza.