1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Donald Tusk kukutana na wenzake wa Ulaya kuijadili Ukraine

9 Novemba 2024

Waziri Mkuu wa Poland Donald Tusk, atakutana na baadhi ya viongozi wa Ulaya kuzungumzia ushirikiano wa kimaeneo pamoja na vita vya Ukraine.

Serba I Belgrade - Aleksandar Vucic na Donald Tusk
Waziri Mkuu wa Poland, Donald Tusk (kushoto) na Rais Aleksandar Vucic wa Serbia.Picha: Darko Vojinovic/AP/picture alliance

Tusk, atakutana na Emmanuel Macron wa Ufaransa, Waziri Mkuu wa Uingereza Kier Starmer, Kiongozi wa Jumuiya ya kujihami NATO Mark Rutte na viongozi wengine wa mataifa ya Nordic na Baltic kwa mazungumzo hayo. 

Hatma ya msaada kwa Ukraine ni miongoni mwa maswali makubwa yanayoulizwa na Umoja wa Ulaya baada ya ushindi wa Donald Trump katika uchaguzi wa Marekani.Trump alikosoa kiwango cha msaada Marekani inayotoa kwa Ukraine katika vita vyake kupinga uvamizi wa Urusi nchini humo, na kabla ya uchaguzi aliahidi kumaliza mzozo huo bila ya kutoa maelezo zaidi.

Josep Borrell afanya ziara fupi Kyiv

Tusk amesema ni wazi hali mpya ya siasa za ulimwengu ni changamoto kubwa kwa kila mtu hasa katika muktadha wa uwezekani wa kusitisha vita vya urusi na Ukraine na pia makubaliano ya Vladimir Putin na rais mteule wa Marekani, Donald Trump.