1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Dortmund yabanwa na Schalke, wafifishwa matumaini ya ubingwa

12 Machi 2023

Borussia Dortmund imeteleza katika mbio za kuwania ubingwa wa Ligi Kuu ya soka Ujerumani, Bundesliga, baada ya kutoka sare ya 2-2 jana na watani wao wa jadi Schalke 04.

Fußball Bundesliga | Schalke 04 vs Borussia Dortmund | Kenan Karaman
Picha: David Inderlied/dpa/picture alliance

Borussia Dortmund imeteleza katika mbio za kuwania ubingwa wa Ligi Kuu ya soka Ujerumani, Bundesliga, baada ya kutoka sare ya 2-2 jana na watani wao wa jadi Schalke 04 katika mechi ya kusisimua iliyochezwa uwanjani Veltins Arena.

Nico Schlotterbeck na Raphael Guerreiro waliiweka kifua mbele Dortmund kabla ya Marius Bütler, aliyefunga bao lake la kwanza katika mechi hiyo ya dabi kwa karibu minne na Kenan Karam kusawazisha na kuufanya mchezo huo kuishia sare.

Kocha wa Borussia Dortmund, Edin Terzic, amesema kuwa, waliiruhusu Schalke kurudi mchezoni katika kipindi cha pili na kwamba vijana wa Thomas Reis walionyesha hamu kubwa ya kupata ushindi tofauti na wao.

Mabingwa watetezi Bayern Munich waliifunga FC Augsburg mabao 5-3 katika mechi nyengine ya dabi ya Bavaria na kufungua mwanya wa alama mbili mbele ya Borussia Dortmund.

Timu hizo zitakutana tena katika uwanja wa Allianz Arena mnamo Aprili 1, katika mechi ambayo huenda ikaamua bingwa wa Bundesliga msimu huu.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW