Dortmund yagonga ukuta kumsajili Witsel
2 Agosti 2018Dortmund inaripotiwa kuwa tayari kuzindua kifungu cha ununuzi cha euro milioni 20 katika mkataba wa Witsel , lakini kocha mkuu wa klabu ya Quanjian Paulo Sousa alionekana kuzima uhamisho huo wa nyota huyo wa kombe la dunia katika mktaba wake unaoenda hadi Disemba 2019.
Sijapata taarifa zozote kuhusu uhamisho wa Witsel, hata kutoka katika klabu ama mchezaji mwenyewe," Sousa aliliambia shirika la utangazaji la CGTN nchini China.
"Naelewa kwamba mchezaji huyo ana kifungu cha uhamisho katika mkataba wake, lakini kifungu hicho kinaweza tu kufunguliwa wakati wa dirisha la uhamisho nchini China. Wakati huu ambapo dirisha la uhamisho nchini China limefungwa hapo julai 12, uhamisho hauwezi kufanyika.
"Nina amani kwamba Witsel atarejea. Ni sehemu kamili ya kikosi chetu."
Mmiliki wa klabu ya Quanjian Shu Yuhui amerudia msimamo huo wa Sou