1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Dortmund yapunguza pengo na Bayern

21 Machi 2016

Timu inayoshikilia nafasi ya pili kwenye ligi Borussia Dortmund ilipunguza uongozi wa Bayern Munich kileleni hadi pointi tano hapo jana, baada ya kutoka nyuma na kuibamiza Augbsurg 3-1.

Fußball 1. Bundesliga FC Augsburg - Borussia Dortmund
Picha: picture alliance/GES/A. Scheuber

Ni ushindi ambao kocha Thomas Tuchel alisema ulikuwa mgumu kwa sababu Dortmund walikuwa bado na uchovu kutokana na mchuano wa Europa League Alhamisi iliyopita dhidi ya Tottenham Hotspurs. Roman Burki ni mlinda mlango wa BVB "Tulipambana sana kucheza katika kipindi cha kwanza. Tulikuwa na makosa mengi maana hatukutulia. Lakini katika kipindi cha pili tukaimarisha kasi. Ilikuwa salama kusawazisha kabla ya kabla ya mapumziko. Mwishowe tukaweza kupata ushindi kutokana na mchezo tulioudhibiti.

Kichapo hicho kimeiacha Augsburg juu ya eneo la kushushwa daraja kutokana na tofauti ya mabao. Bayer Leverkusen ilirejea katika kinyang'anyiro cha kutafuta tikiti ya kucheza Champions League msimu ujao, kwa kuiduwaza Stuttgart 2-0 na kuwaingiza katika nafasi sita za mwanzo. Julian Brandt ni mshambuliaji wa Leverkusen "Tulikuwa tu kama timu uwanjani na tukuweza kutumia nafasi zetu lakini sio zote. ningeweza kufunga goli moja au mawili zaidi. Lakini tulikuwa sawa katika ulinzi na kushambulia langoni, na kisha tukashinda mchezo, ni hivyo tu".

Bayern Munich wanatafuta kushinda taji la Bundesliga kwa mara ya nne mfululizoPicha: Reuters/W. Rattay

Leverkusen sasa wako pointi sawa na nambari tano Borussia Moenchengladbach na pointi mbili nyuma ya Schalke, ambao wako katika nafasi ya nne. Siku ya Jumamosi, bao la 25 la Robert Lewandowski msimu huu liliwapa viongozi Bayern Munich ushindi wa 1-0 dhidi ya Cologne. Lewandoski alikiri mchuano ulikuwa mgumu "Nadhani katika kipindi cha kwanza tulicheza vizuri sana na tukaudhibiti mpira. Cologne haikuwa na nafasi ya kufunga, nadhani tulihitaji leo kufunga na la pili. Ilitutatiza kidogo maana Cologne ili pambana mpaka dakika ya mwisho, lakini baada ya dakika 120 za Champions League, sio rahisi kucheza.

Hertha Berlin inaendeleza matumaini yake ya kucheza Champions League kwa mara ya kwanza tangu 1999/2000 baada ya ushindi wa 2-1 dhidi ya Ingolsdtat, na hivyo kujiimarisha katika nafasi ya tatu, na pengo la pointi nne dhidi ya Schalke.

Wolfsburg imesalia katika nafasi ya nane, baada ya kulazimisha sare ya 1-1 dhidi ya Darmstadt. Katika vita vya kuepuka kushushwa ngazi, Hoffenheim ilipata ushindi muhimu wa 3-1 dhidi ya Hamburg wakati Eintracht Frankfurt ikiizaba Hanover 1-0.

Mwandish: Bruce Amani/AFP/AP/DPA/reuters
Mhariri: Saumu Yusuf

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW