1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Dortmund yawatetea wachezaji kwa kutovaa barakoa

Deo Kaji Makomba
4 Juni 2020

Sancho mwenye umri wa miaka 20 pamoja na wenzake walikwenda saluni kunyoa nywele na kisha kupiga picha wakiwa na kinyozi bila ya kuvaa barakoa.

Deutschland Bundesliga - SC Paderborn v Borussia Dortmund | Jadon Sancho 'Justice for George Floyd'
Msahambuliaji wa kikosi cha Borussia Dortmund Jadon SanchoPicha: Reuters/L. Baron

Kufuatia sakata la wachezaji wa klabu ya soka ya Borussia Dortmund kwenda saloni kuonyoa nywele na kisha kupiga picha na wakiwa hawajavaa barokoa, huku kitendo hicho kikizua gumzo, uongozi wa klabu hiyo umesema itifaki ya usalama wa afya ya Bundesliga haikuvunjwa wakati wachezaji hao akiwemo mchezaji wa timu ya taifa ya England, Jadon Sancho, wiki hii kufanya tukio hilo.

Sancho mwenye umri wa miaka 20, nyota anayeinuka na shabaha ya juu ya uhamisho kwa vilabu vikubwa kutaka kumsajili pamoja na wachezaji wenzake wa klabu hiyo inayoshikilia nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi ya Bundesliga, walikwenda saluni kunyoa nywele na kisha kupiga picha wakiwa na kinyozi bila ya kuvaa barakoa kitu ambacho kinakwenda kinyume na miongozo ya usalama wa afya ya ligi hiyo.

"Hapaswi kuifanya," mkurugenzi wa michezo wa Dortmund Michael Zorc aliuambia mkutano wa wandishi wa habari unaofaa."Sote tulikuwa vijana mara moja, 18, 19, 20." 

"Katika hali hii maalum ya sasa sio tu kuwa mkufunzi na wafanyakazi wa kufundisha bali ni klabu nzima ambayo inapaswa kuwa waangalifu na nidhamu.

"Tumeongea na wote waliohusika na walituhakikishia kwamba miongozo yote ya usafi kuhusu wageni ilizingatiwa. Kwa picha tu ndio barakoa ziliondolewa. Hilo ni jambo ambalo halipaswi kutokea."

Bundesliga imekuwa ni ligi kuu ya kwanza ya soka barani Ulaya kuanza tena Mei 16 baada ya mapumziko ya zaidi ya miezi miwili kufuatia mripuko wa janga la COVID-19.

Mechi zinachezwa bila mashabiki na timu lazima zifuate miongozo madhubuti ya afya ambayo inadhibiti mchakato na uendeshaji wa mazoezi na mechi. Bundesliga, ikiwa na michezo mitano iliyobaki ya msimu huu, imepanga kumaliza mechi zake mwishoni mwa mwezi huu.

Chanzo/RTRE

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW