1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

DOUALA: Hakuna alienusurika katika ajali ya ndege

8 Mei 2007

Tume za waokoaji zikiendelea kusaka mabaki ya ndege ya abiria ya shirika la Kenya Airways, ripoti zinasema,hakuna alienusurika.Siku ya Jumamosi,ndege aina ya Boeing 737-800 ikiwa na watu 114 ilianguka katika eneo la kinamasi,muda mfupi baada ya kuondoka uwanja wa ndege wa Douala nchini Cameroon.Sababu ya ajali hiyo bado haijulikani,lakini kwa vile ndege hiyo iliondoka wakati wa hali mbaya ya hewa,inasemekana huenda ikawa ilipigwa na radi.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW