1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Dozi milioni 10 za malaria zimepelekwa Afrika

23 Januari 2025

Ushirikiano wa Kimataifa wa Chanjo, Gavi umesema karibu dozi milioni 10 za Malaria zilipelekwa barani Afrika katika mwaka wa kwanza wa utoaji wa kawaida wa chanjo kote barani humo.

Symbolbild Malaria | Spritze
Mhudumu wa afya akitayarisha chanjo ya Malaria katika hospitali ya Kaunti ndogo ya Yala, nchini Kenya.Picha: Brian Ongoro/AFP

Gavi amesema zaidi ya dozi milioni 9.8 zimetolewa, na kusema angalau watoto milioni tano wamepata ulinzi wa kutosha.

Soma pia: Ugonjwa wa Malaria waongezeka kwa kasi Rwanda

Kulingana na Gavi, programu hiyo inalenga kutoa chanjo nne kwa kila mtoto na kusisitiza kwamba kila mara ulilenga kuwafikia watu wanaokabiliwa na kitisho zaidi katika kila nchi.

Shirika la Afya ulimwenguni, WHO limesema ugonjwa wa Malaria huua karibu watu 600,000 kwa mwaka, wengi zaidi kutoka Afrika, na waathirika wakubwa wakiwa ni watoto.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW