1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tshisekedi awasilisha fomu ya kuwania urais

8 Oktoba 2023

Rais Felix Tshisekedi wa DRC amewasilisha fomu yake ya kuwania muhula wa pili madarakani, akijiunga na orodha refu ya wagombea wengine, wakiwemo viongozi wa upinzani na mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel, Denis Mukwege.

Felix Tshisekedi Präsident DR Kongo
Picha: Isa Terli /AA/picture alliance

Tshisekedi, ambaye aliingia madarakani kwa mara ya kwanza baada ya uchaguzi mwaka 2018, aliwasilisha rasmi fomu hiyo kutaka ridhaa ya kutumikia muhula wa pili wa miaka mitano katika mji mkuu taifa hilo, Kinshasa.Kujitokeza kwa wagombea wengi wa upinzani kumkabili Tshisekedi, kunatajwa na baadhi ya wachambuzi kwamba kunampa nafasi kubwa kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 60 kuibuka na ushindi.Kongo, taifa lenye eneo kubwa zaidi na misukosuko mingi zaidi katikati ya Afrika, linatarajiwa kufanya uchaguzi wake mkuu Desemba 20 mwaka huu.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW