Kongo, Rwanda zashutumiana majibizano ya risasi mpakani
16 Februari 2023Rwanda limesema wanajeshi kati ya 12 na 14 wa Kongo waliingia katika eneo linalozitenganisha nchi hizo mbili, na kuongeza kuwa mwanajeshi wa Kongo alifyatua risasi kwenye kituo chao cha mpakani.
Katika kujibu tuhuma hizo, gavana wa mkoa wa Kongo wa Kivu Kusini, Theo Ngwabidje, alizitaja kuwa ni uongo, lakinialithibitisha kwamba tukio limetokea mpakani.
Soma pia:Mlinda amani wa UN auawa Kongo
Hata hivyo alilielezea tukio hilo kama ugonvi uliohusisha ufyatulianaji wa risasi kati ya vikosi vya Kongo na wahalifu waliokuwa wanakimbia.
Tukio hilo limejiri katikati mwa mzozo kuhusiana na mashambulizi ya kundi la M23 kwenye mkoa wa Kivu Kaskazini.
Serikali mjini Kinshasa inaituhumu Rwanda kwa kuwaunga mkono wapiganaji hao, madai ambayo yanaungwa mkono pia na wataalam wa Umoja wa Mataifa na mataifa kadhaa ya magharibi, lakini yakipingwa vikali na Kigali.