1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

DR Kongo yaanza kutoa chanjo dhidi ya mripuko mpya wa Ebola

15 Septemba 2025

Shirika la Afya Duniani, WHO, limesema utoaji chanjo kwa watu walio kwenye hatari ya kupata maambukizi ya ugonjwa wa Ebola umeanza jana Jumapili kusini mwa jimbo la Kasai nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo.

DR  Kongo | WHO | Ebola |
DR Kongo yaanza kutoa chanjo dhidi ya mripuko mpya wa Ebola Picha: Olivia Acland/REUTERS

Mripuko wa ugonjwa huo hatari uliripotiwa mapema mwezi huu kwenye kitongoji cha Bulape na kusababisha vifo vya watu 16 na wengine 68 wanashukiwa kuwa wameambukizwa.

WHO imesema dozi za awali zipatazo 400 za chanjo aina ya Ervebo zimetolewa na shehena nyingine ya chanjo itapelekwa siku chache zinazokuja.

Miongoni mwa wanaopatiwa chanjo hizo ni maafisa wa afya walio mstari wa mbele na watu wanaoaminika huenda watapata maambukizi kutokana na ukaribu wao na waliokwishaambukizwa.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW