1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Dramani Mahama ashinda uchaguzi Ghana

9 Desemba 2024

Rais wa zamani wa Ghana John Dramani Mahama anatarajiwa kurejea madarakani baada ya mgombea wa chama tawala katika uchaguzi wa urais nchini humo, Makamu wa Rais Mahamudu Bawumia, kukubali kushindwa katika uchaguzi huo.

Ghana I Wahlen
Picha: Misper Apawu/AP/picture alliance

Kabla ya tangazo rasmi, Bawumia aliwaambia waandishi wa habari kwamba anaheshimu uamuzi wa raia wa nchi hiyo na kusema kuwa tayari amempigia simu Mahama kumpongeza kama rais mteule wa nchi hiyo.

Katika ujumbe alioandika mwenye mtandao wa X, Mahama mwenye umri wa miaka 65 na ambaye aliwahi kuwa rais wa nchi hiyo kati ya Julai 2012 na Januari 2017, alithibitisha kuhusu mawasiliano yake na Bawumia na akautaja ushindi wake kuwa wa kishindo.

Wakati wa kampeni yake, Mahama aliahidi kufanya marekebisho katika sekta mbali mbali za nchi na kutoa kipaombele kwa uchumi, hivyo basi akawavutia vijana waliouona uchaguzi huo kama njia ya nchi hiyo kujikwamua kutoka kwa mgogoro wa kiuchumi.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW