1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

DRC: Chuo cha mafunzo ya kivita chazinduliwa

Jean Noel Ba-Mweze6 Januari 2021

Rais Felix Tshisekedi amezindua chuo cha mafunzo ya kivita mjini Kinshasa, chuo hicho kinadhaminiwa na serikali ya Ufaransa kinalenga kuwapa elimu ya hali ya juu maafisa wa jeshi nchini humo ili kuboresha hali ya usalama

Mai-Mai Milizen im Kongo
Picha: Dai Kurokawa/dpa/picture alliance

Ripoti ya Umoja wa Mataifa imeyalaumu makundi yanavyomiliki silaha, na pia jeshi na polisi kwa ukikuaji wa haki za binadamu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Wakongomani wanakubali umuhimu wa kuwepo chuo cha mafunzo ya kivita hapa nchini, ila wengi wao, hususan wakaazi wa maeneo yanayokumbwa na mashambulizi wanasema suluhisho la haraka ndiyo kitu muhimu zaidi, ili kurejesha hali ya usalama.

Soma zaidi: DRC: Watu 25 wauawa na waasi mkesha wa Mwaka Mpya

Usiku wa kuamkia jana Jumanne ambapo chuo hicho kilizinduliwa, kulikuwa na mauwaji mengine yaliyofanywa na watu wanaodhaniwa kuwa waasi wa ADF kutoka Uganda katika mji wa Beni mkoani Kivu ya kaskazini mashariki mwa nchi, jambo lililomkasirisha mbunge maalum Muhindo Vaomawa wa Beni.

"Ni watu 23 ndiwo waliuwawa usiku huo. Mimi naomba rais asingoje kuwepo na serikali ya muungano wa taifa ili ajihusishe na usalama wa raia. Hali huko Beni ni udhalilishaji dhidi yake rais, dhidi ya bunge, dhidi ya serikali na dhidi ya jeshi. Mimi nawaza inakuwa haraka."

Hali kama hiyo ipo pia mkoani Ituri kaskazini mashariki mwa Kongo ambako wakaazi wanakabiliwa na usalama mdogo.

Makundi yanayomiliki silaha yanaendelea kuwashambulia raia

Picha: Alexis Huguet/AFP/Getty Images

Makundi yanayomiliki silaha yanaendelea kuwashambulia na kuwauwa raia kila mara. Mashirika ya kiraia yanasema hata chuo hicho cha mafunzo ya kivita hakitaweza kuya yatatua matatizo ya Ituri mara moja bali, kinachohitajika suluhisho la haraka. Dieudonnee Lossa Dhekana ni kiongozi wa shirika la kiraia mkoani humo.

"Chuo cha kivita hakitaitatua shida tunayo. Kwa sasa, tunahitaji huduma. Kwa sasa tunahitaji vita kusitishwa. Chuo cha kivita kitaanza wakati raia wa Ituri wote tayari wamekimbia ? Tunachokihitaji ni suluhisho la haraka, ili kuyakomesha mauwaji ya raia hapa Ituri."

Ripoti mbalimbali za umoja wa mataifa kila mara zimelilaumu jeshi na polisi kwa kuhusika na vitendo vya ukikuaji wa haki za binadamu. Kuna matumaini kwamba chuo cha kivita kitawasaidia maofisa kujua jinsi ya kuchunguza mwenendo wa vikosi vyao, kama alinasema Abdoul Aziz Tioye, mwakilishi wa ofisi ya umoja wa mataifa husikayo na haki za binadamu.

"Chuo cha kivita kitawaruhusu maofisa kujihami kwa elimu na ujuzi, ili ya kuongoza vyema na kuchunguza ipasavyo vikosi chini ya uongozi wao. Ni muhimu vikosi kuwa na nidhamu na hivyo kuboresha mwenendo kazini na kwenyi mapambano, yaani askari kuziheshimu haki za binadam."

Katika hotuba zake mbalimbali, rais Felix Tshisekedi ameahidi kufanya liwezekanalo ili kuirejesha Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo katika hali ya usalama.

 

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW