1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

DRC kuanza kampeni ya chanjo dhidi ya malaria

28 Oktoba 2024

Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo kesho Jumanne itaanza kampeni ya kutowa chanjo dhidi ya ugonjwa wa Malaria. Hayo yalitangazwa na Shirika la Afya Duniani, WHO wiki iliyopita.

Anofelesi | Malaria
Mbu aina ya anoflesi jike anayeambukiza ugonjwa wa MalariaPicha: RealityImages/Zoonar/picture alliance

Taarifa ya ujumbe wa WHO unaohusika na nchi hiyo ya Afrika ya Kati, imesema wizara ya afya ya Kongo itaanzisha kampeni hiyo kwa mara ya kwanza Oktoba 29 ambapo chanjo za mwanzo zitatolewa katika mkoa wa Kongo Central uliko Kusini Magharibi mwa nchi hiyo.

Chanjo hiyo ya R 21/ Matrix M inakusudiwa kutolewa kwa watoto wadogo wa umri wa miezi 6 hadi 23. 

Malaria ni maradhi yanayoweza kusababisha kifo na inasambazwa kwa binadamu kupitia aina maalum ya mbu. Chanjo hiyo pia ilishaanza kutolewa katika nchi nyingine za Afrika zikiwemo Kenya, Cameroon, Malawi na Benin.