1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

DRC kuhamisha ubalozi wake wa Israel hadi Jerusalem

22 Septemba 2023

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, itahamisha ubalozi wake nchini Israel, kutoka mji wa Tel Aviv hadi mji wa Jerusalem.

Felix-Antoine Tshisekedi
Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Felix TshisekediPicha: Leonardo Munoz/AFP/Getty Images

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, itahamisha ubalozi wake nchini Israel, kutoka mji wa Tel Aviv hadi mji wa Jerusalem.

Hayo yamesemwa leo Ijumaa na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu, aliyekutana na rais wa Congo Felix Tshisekedi wakati wa Hadhara Kuu ya Umoja wa Mataifa. Alitangaza pia kuwa Israel itafungua ubalozi wake Kinshasa, mji mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Ni nchi chache pekee ndizo zina ofisi zao za ubalozi mjini Jerusalem. Mataifa mengi yameweka ofisi zao za kidiplomasia katika mji wa bandari Tel Aviv ambao pia ni kitovu cha uchumi cha Israel.

Soma pia: Ubalozi wa Marekani wahamishiwa Jerusalem kutoka Tel Aviv

Japo Israel huchukulia Jerusalem kuwa mji wake mkuu usiogawika na hutaka nchi kuweka ofisi zao za ubalozi mjini humo, sehemu kubwa ya dunia bado haitambui mamlaka ya Israeli juu ya mji mzima wa Jerusalem, na huamini kwamba mzozo juu ya mji huo unapaswa kutatuliwa kwa njia ya mazungumzo.

Wapalestina wanautaka mji wa Jerusalem kuwa jimbo lao huru la eneo la mashariki ambalo Israel lilikamata wakati wa vita vya mwaka 1967 vya Mashariki ya kati yake.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW