Maadhimisho ya miaka 55 ya Uhuru
30 Juni 2015Matangazo
Rais Kabila ambae amelihutubia taifa katika madhimisho ya miaka 55 ya uhuru wa Kongo leo , amesema kwamba uchaguzi ujao utakuwa wa utulivu na amani , huku akiwaomba wapinzani kushiriki kwenye mazungumzo ya kitaifa ili kujadili changa moto za uchaguzi.Hata hivyo Kabila ambaye hakutaja ikiwa atagombea au la, ametupilia mbali pendekezo la kuweko na msuluhishi wa kimataifa katika mazungumzo hayo kama wanavyodai wapinzani.
Taarifa kamili na mwandishi wetu Saleh Mwanamilongo.
Mwandishi Saleh Mwanamilongo
Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman