1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroAfrika

DRC: Maelfu wakimbia baada ya M23 kuingia Sake

23 Januari 2025

Hali ya wasiwasi inaendelea kutanda katika mji wa Goma, ambapo maelfu ya watu wanakimbia kutokana na mapigano makali kati ya jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na waasi wa M23.

Waasi wa M23 wameuteka mji wa Minova
Wakaazi walioachwa bila makazi wakifunga safari kwenda Goma wakitoka kwenye mji wa Minova, Kivu KusiniPicha: ALEXIS HUGUET/AFP

Wakati waasi hao, wanaoungwa mkono na jeshi la Rwanda, wakiteka mji wa SAKE, wakazi wengi wanajikuta wakiwa na hofu na kukosa mahali pa kwenda.

Wakazi wameketi kando ya barabara wakiwa na mifugo na mizigo yao, bila kujua hatima yao. Hali hii inatokana na kuongezeka kwa ghasia na mapigano, ambapo waasi wa M23 wamefanikiwa kuteka mji wa Sake, umbali wa kilomita 20 kutoka Goma. Raia wanaokimbia kutoka katika baadhi ya makambi karibu na mji wa Goma wakihofia usalama wao wanasema. Tayari waasi hao wameukamata mji muhimu wa Minovaulioko Kongo Mashariki. 

M23 wazidi kuisogelea Goma huku wasiwasi ukitanda

01:48

This browser does not support the video element.

Jeshi la Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Kongo hata hivyo linashambulia kwa mizinga maeneo yote yanayozungukwa na mji huo wa sake ambamo raia wote wamekimbia. Huku waasi wakisonga mbele wakipiga roketi kuelekea sasa kijiji cha Mubambiro karibu na kambi za wakimbizi mjini Goma. Aline KAHINDO bado anahangika kupata sehemu ya kukimbilia.

Janvier MAPENZI ni mwanaharakati wa asasi za kiraia mashariki mwa kongo. Wakazi wa Goma wanakabiliwa na changamoto kubwa, huku njia nyingi zikifungwa kutokana na mapigano, na wengi wanalazimika kuvuka Ziwa Kivu kwa njia hatari ili kutafuta hifadhi Hali ambayo inawatia wasiwasi mkubwa wananchi wa Goma. Hadi Jumatano jioni, anga la mji wa Sake limejaa ndege za kivita zinazovurumisha mizinga kwenye mji huo wa kimkakati huku milio ikianza kusikika magharibi mwa mji wa Goma ambamo shughuli zote zimekwama tangu asubuhi.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW