Martin Fayulu akataa mwito wa maridhiano wa Tshisekedi
3 Februari 2019Matangazo
Mwito huo wamaridhiano umetolewa na rais mpya wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo katika jitihada ya kutafuta maridhiano ya kisiasa nchini humo. Fayulu amesema pale unapopewa mkono ambao ni mchafu, hupaswi kuupokea.
Kwenye hotuba yake rasmi ya kwanza tangu kushindwa kwenye uchaguzi wa rais, Fayulu aliwaambia mamia ya wafuasi wake waliokusanyika mjini Kinshasa, kuwa awasifanye fujo wakati anapoendelea kupinga uchaguzi anaodai ulikumbwa na udanganyifu. Kiongozihuyo wa upinzani ameuhimiza Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika kutopokea maagizo kutoka kwa mtu anayedai kuwa Wakongo hawakumchagua.
Mwandishi:John Juma/DPAE
Mhariri: Zainab Aziz