1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

DRC: Mgawanyiko waukumba muungano wa rais mstaafu Kabila

Jean Noel Ba-Mweze21 Desemba 2020

Muungano wa vyama vilivyo upande wa rais mustaafu nchini DRC Joseph Kabila, FCC, unaendelea kugawanyika baada ya wabunge kumpindua Jeanine Mabunda, aliyekuwa spika wa bunge toka Chama chake Kabila.

Demokratische Republik Kongo Parlament in Kinshasa
Picha: Getty Images/AFP/J. D. Kannah

Baadhi ya vyama vinavyounda muungano huo huwalaumu wakuu viongozi wa FCC kwa kuongoza kwa upendeleo na ubaguzi hadi kuangusha muungano huo. Upande wao raia wengi wanawaza kwamba mugawanyiko huo unakuja kuifuta kabisa FCC.

Tangu kuondolewa kwake Jeanine Mabunda katika nafasi ya spika wa Bunge la jamhuri, muungano wa kisiasa wa Joseph Kabila, FCC unakumbwa na hali ya vurugu miongoni mwa wanachama.

Wengi waliomba kujiuzulu kwake Nehemie Mwilanya ambae ni mratibu wa FCC, pamoja na viongozi wengine wakiwemo Evarist Boshab, Ramazani Shadary, Aubin Minaku, Adolphe Lumanu na wengine.

Ushawishi wa Joseph Kabila wazidi kushuka kisiasa DRC?

This browser does not support the audio element.

Watu hao wanawekwa sasa kando, kama alivyotangaza Evani Ilunga Ngindu toka chama cha ANADEC na ambae ametangaza kuanzishwa kwa muungano uitwao FCC progressiste. 

"ANADEC inatangaza kuanzishwa kwa muungano wa kisiasa ujulikanao kama FCC progressiste. Muungano huu unawaletea matumaini wale wote waliobaguliwa, waliowekwa kando na ambao hawakushugulikiwa kutokana na upendeleo. Lengo ni kuulinda wingi wa kambi ya kisiasa ya joseph kabila." Amesema Evani Ilunga Ngindu

Soma pia: Rais Tshisekedi kuuvunja ushirikiano na upande wa Kabila

Kuundwa kwa kundi hilo lililojiengua kutoka muungano wa FCC ambalo hakutambuliwi na baadhi ya vyama vingine vinavyomuunga mkono Kabila, vinavyosema kwamba tangazo hilo limetolewa na chama kimoja wala halijulikani na vyama vingine.

Tangu wiki iliyopita, tayari miungano minne iliyomevuka kutoka FCC imetangazwa nayo ni FCC Renaissance, FCC Renovateur, FCC Republicain na FCC Progressiste.

Hali ya kisiasa ya Congo ndio tunayoijadili katika Maoni

This browser does not support the audio element.

Raia wengi tuliokutana nao wanawaza kwamba mgawanyiko huo unajitokeza kwa lengo la faida za kibinafsi, na ndio unakuja kuisambaratisha kabisa FCC.

Mzozo wa siasa DRC wazidi kuibua wasiwasi

"Mimi nawaza huo ndio mwisho wa muungano huo wa kisiasa kwani mugawanyiko unakuja kuzimaliza nguvu waliokuwa nazo. Tusubiri tuone ila mimi nawaza huo ni mwisho. Kunakuwa FCC nyingi na hawataungana tena. Ni watu ambao wanaona tu faida zao binafsi. Wangelijishughulisha na faida za raia hawangegawanyika. Moja akiona mwengine anapata naye anataka pia apate. Wote wanafuata tu faida za kibinafsi na zisizoambatana na maendeleo ya Kongo yetu." Ni maoni ya raia ambaye hakujitambulisha jina.

Siku hizi wengi miongoni mwa wanachama wa FCC wanauhama muungano huo wake Joseph Kabila ili kujiunga na muungano wa taifa ulioundwa naye rais Felix Tshisekedi.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW