DRC: Mwanamuziki Pepe Ndombe Opetum afariki dunia
25 Mei 2012Matangazo
PEPE NDOMBE OPETUM naibu kiongozi wa bendi ya Bana Ok amekufa akiwa na umri wa miaka 68. Alipata umaarufu wakati alipokuwa akiimba na Hayati Luwambo Makiadi na Lutumba Simaro . Wimbo wake wa MOKOLO NA KOFUFA (Siku nitakayo fariki) ndio maarufu sana katika eneo la Afrika Mashariki na Kati na uliompandisha kwenye jukwaa la waimbaji bora wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo.
Saleh Mwanamilongo kutoka Kinshasa anaarifu zaidi juu ya kifo cha Pepe Ndombe
(Kusikiliza ripoti hiyo bonyeza alama ya spika za masikioni)
Mwandishi: Sudi Mnette
Mhariri: Saleh Mwanamilongo