DRC: Vituo 38 vya Radio na Televisheni vyapigwa maarufu
22 Oktoba 2007Matangazo
Hatua hiyo imechukuliwa na waziri wa habari wa nchi hiyo ambaye amewalaumu viongozi wa vituo hivyo kwa kutodumisha nidhamu na vituo vingine vimekuwa vikiendeleza kazi zake bila leseni ya utangazaji.
Shirika la kutetea haki za waandishi wa habari nchini humo limepinga vikali hatua hiyo.
Mwandishi wetu Saleh Mwanamlongo anaripoti zaidi kutoka Kinshasa.