DRC: Wakaazi wataka mamlaka kukabidhi maiti kwa familia zao
14 Septemba 2023Vifo vya hivi karibuni vilivyotokea mjini Goma tarehe 30 Agosti katika maandamano dhidi ya ujumbe wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemocrasia ya Kongo MONUSCO, vimeacha familia nyingi zikiwa na huzuni kubwa, huku wanavumilia maumivu yasiyoisha.
Baada ya wiki mbili,bado familia za wahanga wanangojea kupewa miili ya watu wao kuwazika kwa heshima.
Kwa bahati mbaya, miili haikuwahi kupelekwa katika vyumba vya kuhifadhi maiti, jambo linaloongeza hatari ya kuoza kwa miili hiyo.
Soma pia:Makamanda wawili wa jeshi wakamatwa Congo
Baadhi ya familia za wahanga waliopoteza maisha katika maandamano hayo, wameiambia DW kwamba, wanachohitaji kwa sasa ni miili hiyo kwa ajili ya shughuli za mazishi.
"Tunahitaji kuzika kwa heshima jamaa zetu." Alisema Laetitia Mazino katika mahopjiano na mwandishi wa Dw mjini humo.
Wakaazi hao wameitaka serikali kuingilia kati ili kumaliza kadhia hiyo ambayo wameitaja ni hatari pia kwa wakaazi wanaozunguka kambi hiyo, kutokana na miili hiyo kutohifadhiwa kwa kufuata miongozo ya afya.
Mashirika ya kiraia yaingilia kati
Miili ya wahanga wote iko nyuma ya kambi ya kijeshi ya Goma, imerundikwa ndani ya kontena. Hakuna aliyezikwa bado.
Kwa mujibu wa mashirika la kiraia ya Goma, miili hiyo ambayo imeanza kuharibika inaleta hatarikubwa kwa afya ya watu wanaoishi karibu na kambi hii.
Marrion Ngavo, mkuu wa shirika la kiraia la Goma, anaiomba serikali iheshimu utu wa binadamu kwa kuzika miili hii.
Soma pia:Watu wasiopungua kumi wauawa katika maandamano mjini Goma
Zaidi ya watu 130 wamekamatwa katika kesi hii na kufikishwa mbele ya mahakama katika kesi ya kisheria tangu wiki iliyopita.
Wito wa kutaka hatua zichukuliwe unazidi kuongezeka mjini Goma, na kuna matumaini kutoka kuchukua hatua kwa kutoa miili hiyoi kwa familia zao.