DRC: Wanamuziki chipukizi waimba kwa ajili ya watoto
4 Julai 2012Matangazo
Mradi huo wa pamoja utafadhiliwa na mashirika ya kimataifa yakiwemo Shirika la Watoto la Umoja wa Mataifa, UNICEF na Shirika la Msalaba Mwekundu. Fedha zitakazotoka baada ya kuuza wimbo huo zitatumiwa kwenye miradi ya elimu na huduma za kiafya za watoto yatima. Hata hivyo kuimba pamoja kwa Ferre Gola na Fally Ipupa kumezusha maoni mengi kwa mashabiki wao kuhusu nani mwanamuziki bora. Taarifa kamili na mwandishi wetu mjini Kinshasa Saleh Mwanamilongo.
(Kusikiliza taarifa hiyo bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini)
Mwandishi: Saleh Mwanamilongo
Mhariri: Abdul-Rahman Mohammed