DRC: Waziri wa zamani wa afya ahojiwa kuhusu fedha za Ebola
28 Agosti 2019Waziri wa zamani wa afya aliyejiuzulu mwezi uliopita katika jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo Oly Ilunga amehojiwa jana na mwanasheria mkuu wa serikali kujibu masuala kuhusu jinsi fedha za umma zilizolengwa kwa ajili ya kupambana na maradhi ya Ebola zilivyotumika.
Wakili wake Guy Kabeya ameliambia shirika la habari la Ufaransa AFP, Dr.Ilunga ametoa ushahidi na kwamba ana imani na mfumo wa sheria wa nchi yake.
Duru za mahakama zimesema Dr. Ilunga aliachiwa baada ya mahojiano kumalizika.
Washauri wake watatu wa zamani, akiwemo tabibu mmoja wangali bado wanashikiliwa rumande.Dr. Ilunga amejiuzulu julai 22 iliyopita baada ya kupokonywa wadhifa wa kuongoza juhudi za kupambana na Ebola.
Maradhi ya Ebola yameangamiza maisha ya katibu watu 2000 katika jamahurib ya kidemokrasi ya Kongo.