1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

DRC yadai askrai 500 wa Rwanda wameingia nchini mwake

9 Juni 2022

Jeshi la Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo limetangaza kuweko upya kwa askari zaidi ya 500 waliovuka mpaka kutoka Rwanda kuingia Kongo kupitia milima ya Chanzu, eneo la mapigano kati ya jeshi la kongo na waasi wa M23.

Kongo Brazzaville | Kongolesische Soldaten
Picha: Jerome Delay/AP/picture alliance

Katika taarifa yake ya jana jioni, jenerali Sylvain Ekenge ambaye ni msemaji wa gavana wakijeshi hapa Kivu ya Kaskazini amefahamisha hayo wakati alipokua akiwafahamisha waandishi wa habari kuhusu wanajeshi wa Rwanda walioingia upya nchini Kongo na walioonekana kwenye milima ya Chanzu wilayani Rutshuru wakiwa wamevalia sare aina mpya tofauti na kama inavyokuwa kawaida kwa askari wa nchi hiyo jirani na Congo.

Rwanda yasema iko tayari kulipiza kisasi iwapo Congo itashambulia tena

Kulingana na ushuhuda wa  wakazi wa maeneo hayo hayo, mamia ya askari wa jeshi la Rwanda walionekana kwenye mizunguko ya  mlima mrefu wa Chanzu ambao umekua ni ngome muhimu ya kundi la waasi wa M23.

Jeshi la Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo limetangaza kuweko askari zaidi ya 500 waliovuka mpaka kutoka Rwanda walioingia nchini mwake.Picha: Moses Sawasawa/AP/picture alliance

Hata hivyo, upande wa viongozi wa mashirika ya kiraia ambayo pia yamethibitisha kuweko kwa askari hao akiwemo Jean Claude Bambanze ambaye ni mkuu wa mashirika ya kiraia wilayani Rutshuru, wamezitaka serikali zote hizo mbili zinazo laumiana kuingia kwenye mazungumzo ili kuondoa tofauti zinazoshuhudiwa hivi sasa.

Kongo yaishutumu Rwanda kuwaunga mkono waasi wa M23

Hali imekuwa ni ya wasiwasi katika baadhi ya maeneo wilayani Rutshuru na nyiragongo ambamo mzozo  huo katika ya nchi hizi mbili umesababisha maelfu ya raia kuvitoroka vijiji vyao ili kupata hifadhi katika makambi nje kidogo na mji wa Goma.

Kwa muda mrefu serikali ya kigali imekuwa ikiilaumu kinshasa kwakuwahifadhi waasi wa FDLR ambao ni tishio kubwa kwa nchi hiyo . katika mazungumzo yake pamoja na  raisi wa angola mapema mwanzoni mwa juma hili, Rais Tshisekedi alithibitisha kuhusu Rwanda  kulisaidia kundi la waasi wa M23 hali inayo endelea kuongeza utata kati ya mataifa haya mawili .