1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

DRC yawazika watu waliouawa kambi ya wakimbizi

15 Mei 2024

Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imefanya mazishi ya miili ya watu waliouawa kwenye mashambulizi ya tarehe 3 Mei 2024 katika makambi ya wakimbizi mjini Goma.

Makambi ya wakimbizi Goma 2024
Watu wakiwa wamekusanyika karibu na kulikotokea mlipuko katika kambi ya wakimbizi GomaPicha: Moses Sawasawa/AP Photo/picture alliance

Ilikuwa siku yenye shughuli nyingi sana mjini Goma, ambapo shughuli zilibaki zimesimama katika nusu ya mji. Mji wote ulikuwa umeshiriki kwa ajili ya kutoa heshima kwa watu hawa waliouawa kikatili na mabomu ya uasi wa M23.

Wakati miili ya waathirika ilipokuwa ikipangwa kwa ajili ya shughuli za heshima, waandamanaji wa harakati za raia walitumia fursa hiyo kufanya maandamano ya hasira mbele ya chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali kuu ya Goma, ambapo sehemu ya waathirika walikuwa wamehifadhiwa.

Kambi ya wakimbizi GomaPicha: Moses Sawasawa/AP Photo/picture alliance

Dav Sikiliza, ni mwanaharakati wa harakati za raia mjini Goma.

"Ni hali ya kukata tamaa kuhusiana na yote yanayotokea. Tunaiomba serikali kuu kulinda raia na kuacha mikakati ya kujihami. Tunapaswa kuchukua hatua ya kushambulia. Ni wakati wa kujibu."

Soma: Rwanda yakanusha shutuma za Marekani kuhusu Kongo

Hii ilifuatiwa na shughuli ya heshima kwa waathirika katika uwanja wa Umoja wa Goma, kwa uwepo wa ujumbe mkubwa uliokuja kutoka Kinshasa, ukiwa na viongozi wakuu sana wa serikali kuu ikiwa ni pamoja na msemaji wa serikali, mawaziri wa haki za binadamu na masuala ya kijamii, na wabunge wa kitaifa. Katika hotuba yake, Waziri Modeste Mutinga waziri wa kitaifa wa masauala ya kijamii alisema; 

Maelfu wakimbia vita Sake

02:42

This browser does not support the video element.

"Hii taswira ya kuhuzunisha na ya kuumiza inathibitisha kikamilifu kiwango cha ukatili na dhima ya Rwanda na kiongozi wake Paul Kagame. Ni kero. Ya kutosha ni ya kutosha. Lazima isimame na itasimama. Rais wa Jamhuri anaendelea kutia bidii ili amani irudi katika sehemu hii ya nchi ambayo inakabiliwa na ukosefu wa usalama."

Fuatilia habari hii: Shambulizi la anga lawaua watu tisa katika kambi ya wakimbizi wa ndani nchini DRC

Waathirika wamezikwa katika makaburi ambayo yamepewa jina la "Kumbukumbu ya GENOCOST", ili kuwakumbuka waathirika wa uvamizi wa Rwanda na kuwakumbusha vizazi vijavyo kwamba vita ilichukua maisha ya idadi kubwa ya raia wasio na hatia.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW