DRC yaifungia Al Jazeera kurusha matangazo yake nchini humo
10 Januari 2025Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo imekifungia kituo cha televisheni cha Al Jazeera kutokana na kurusha mahojiano na kiongozi wa kundi la waasi ambalo limechukua udhibiti kwenye baadhi ya eneo la mashariki mwa nchi hiyo hivi karibuni.
Msemaji wa serikali ya Kongo, Patrick Muyaya amesema mamlaka zimebatilisha kibali cha kurusha matangazo cha televisheni hiyo ya Qatar nchini Kongo, baada ya kurusha mahojiano na mkuu wa kundi la M23, Bertrand Bisimwa.
Soma pia: Congo bans Al Jazeera over its interview with a key rebel leader and threatens journalists
Muyaya amesema Al Jazeera ilirusha mahojiano hayo bila kupata kibali maalum.
Siku ya Jumatano, Al Jazeera ilirusha mahojiano ya Bisimwa, ambapo aliishutumu serikali ya Kongo kwa kukiuka makubaliano ya kusitisha mapigano ya mwezi Agosti.
Aidha, Waziri wa Sheria wa Kongo, Constant Mutamba amesema waandishi habari au mtu yeyote atakayeripoti kuhusu shughuli za jeshi la Rwanda na waasi wa M23, atashtakiwa na kuhukumiwa adhabu ya kifo.