1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

DRC yaipiga Nigeria 4-3 kwa mikwaju ya penalti

17 Novemba 2025

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imezima matumaini ya Nigeria ya kufuzu Kombe la Dunia la 2026 baada ya kushinda kwa mikwaju ya penalti katika mchuano wa mchujo wa Afrika.

Kombe la Mataifa ya Afrika | Ivory Coast - DR Congo
Jamhuri ya Kongo katika Uwanja wa Alassane Ouattara mjini Abidjan, Ivory Coast mnamo Februari 7, 2024Picha: Fareed Kotb/Anadolu/picture alliance

DRC na Nigeria zilitoka sare ya 1-1 baada ya muda wa nyongeza kwenye mchezo uliochezwa Rabat, na timu ya Afrika ya Kati ikashinda kwa penalti 4-3 ili kujihakikishia nafasi ya kushiriki hatua ya mtoanao ya mabara utakaofanyika Mexico mwezi Machi mwaka ujao.Nigeria iko nafasi 19 juu ya DRC kwenye viwango vya FIFA na ilikuwa ikipewa nafasi kubwa kabla ya mechi. Hata hivyo, DRC ilijipanga vyema kwa kadri muda ulivyokwenda ikaonekana kuwa na uwezekano mkubwa wa kushinda.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW