DRC yapata makubaliano ya kisiasa - Upinzani
23 Desemba 2016Kwa mujibu wa rasimu ya makubaliano hayo, ambayo shirika la habari la Reuters limepata nakala yake, sasa Rais Kabila ataondoka madarakani mwishoni mwa mwaka 2017, hatua ambayo haikutarajiwa, hasa baada ya watu zaidi ya 20 kuuawa kwenye maandamano dhidi ya Kabila wiki hii.
Wanasiasa wa upinzani waliozungumza na Reuters wanasema makubaliano hayo "yanamzuia pia Kabila kufanya mabadiliko ya katiba ambayo yangelimruhusu kuwania muhula wa tatu".
Vile vile, pataundwa serikali ya mpito ambayo itasimamiwa na waziri mkuu kutoka kundi la wapinzani lenye nguvu, huku kiongozi mkuu wa upinzani, Etienne Tshisekedi, akipewa jukumu la kusimamia utekelezaji wa makubaliano hayo.
Msemaji wa serikali amekataa kutungumzia chochote kuhusiana na makubaliano hayo, yaliyofikiwa leo chini ya usimamizi wa Kanisa Katoliki nchini Kongo.