1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

DRC yapiga marufuku maandamano ya upinzani

26 Desemba 2023

Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imepiga marufuku maandamano yaliyoitishwa na upinzani yaliyopangwa kufanyika Jumatano 27.12.2023 kupinga hitilafu katika uchaguzi wa wiki iliyopita.

Uchaguzi katika Jamuhuri ya Kidemkrasia ya kongo
Afisa wa Tume Huru ya uchaguzi (CENI) akiangalia kadi ya kupiga kuraPicha: ARSENE MPIANA/AFP

Siku ya Jumamosi, wagombea watano wa urais kutoka upinzani walimfahamisha Mea wa jiji la Kinshasa kuhusu nia yao ya kuandaa maandamano hayo.

Lakini serikali imesema maandamano hayataruhusiwa kwa kuwa matokeo ya uchaguzi bado hayajatangazwa rasmi. Waziri Mambo ya Ndani wa Kongo Peter Kazadi aliwaambia waandishi wa habari kuwa maandamano ya kesho yanalenga kudhoofisha mchakato wa uchaguzi na serikali haiwezi kukubali hilo.

Soma pia:Felix Tshiekedi aongoza katika matokeo ya awali ya uchaguzi wa Rais nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo 

Viongozi wa upinzani walioitisha maandamano hayo ni pamoja na Martin Fayulu ambaye alidai alishinda uchaguzi uliopita mwaka wa 2018, na Denis Mukwege, mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel ambao wamekashifu uchaguzi huo na kuutaja kama kichekesho.

Soma pia: Marekani yatoa wito wa uwazi kwa uchaguzi wa Kongo

Moise Katumbi, mgombea mwingine na gavana wa zamani wa eneo la kusini-mashariki la Katanga, alitaka uchaguzi huo ubatilishwe. Takriban wapiga kura milioni 44, kati ya wakazi wapatao milioni 100 wa Kongo, walipiga kura ya kuchagua rais, wabunge, madiwani na viongozi wa manispaa katika kura za Jumatano iliyopita.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW