DRC yatarajia kutangaza mwisho wa Ebola mwezi April
10 Machi 2020Matangazo
Wakati ulimwengu ukijishughulisha zaidi kwenye mripuko wa virusi vya Corona, mgonjwa wa mwisho aliekuwa anatibiwa Ebola nchini Congo aliruhusiwa Jumanne iliyopita.
Iwapo hakutakuwa na visa vipya, ugonjwa huo utatangazwa kumalizika rasmi Aprili 12, au siku 42 kuanzia tarehe ambapo kipimo cha pili cha mgonjwa wa mwisho kilionyesha hana tena maambukizi.
Afisa anaehusika na mapambano dhidi ya Ebola Jean-Jacques Muyembe, alisema wanatarajia hadi wakati huo, hakutakuwa na matukio mengine ya ugonjwa huo.
Mripuko wa karibuni zaidi wa Ebola nchini Congo uligunduliwa kwa mara ya kwanza Agosti 2018, na shirika la afya duniani WHO, liliutangaza kuwa dharura ya kimataifa ya kiafya Julai mwaka uliyopita.