Dresden, Ujerumani. Matokeo ya uchaguzi SPD yashinda.
3 Oktoba 2005Matokeo rasmi ya kura katika mji wa mashariki ya Ujerumani wa Dresden yametangazwa.
Chama cha Christian Democrats kimepata wingi zaidi, na kuongeza ushindi wao katika viti vya bunge dhidi ya chama cha Social Democrats kwa jumla ya viti vinne .
Hata hivyo , kwa kuwa sheria za uchaguzi nchini Ujerumani zinampa kila mpigakura nafasi ya kura mbili, moja kwa ajili ya mgombea na moja kwa ajili ya chama akipendacho, inaonekana kuwa chama cha SPD cha kansela Gerhard Schröder kimeshinda tena kwa kupata asilimia 28 ikilinganishwa na asilimia 24 kwa chama cha CDU.
Hali hii inaweza kuleta utata zaidi katika mazungumzo ya kuunda serikali ya mseto kati ya vyama hivyo viwili katika kile kinachoitwa muungano mkuu , kwa sababu kila chama kinasisitiza kuwa kinapaswa kukalia kiti cha ukansela.