1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Droni za Ukraine zalenga mitambo ya mafuta na umeme Moscow

1 Septemba 2024

Duru kwa upande wa Urusi zinasema Ukraine imefanya mfululizo wa mashambulizi ya droni kulenga mitambo ya kuzalisha umeme na kusafisha mafuta huko Moscow na eneo la jirani la Tver.

Urusi | Moto wa kusafishia mafuta wa Moscow
Moshi ukifuka kutoka kwa kiwanda cha kusafisha mafuta cha Kapotnya. Picha: IMAGO/ITAR-TASS

Mashambulizi hayo yanaelezwa kusababisha miripuko ya moto, huku taarifa hiyo ikiendelea kusema droni nyingine kadhaa zilifanikiwa kudhibitiwa kuingia katika baadhi ya maeneo ya taifa hilo.

Kupitia ukurasa wake wa telegram wizara ya ulinzi ya Urusiimesema kikosi chake cha ulinzi waanga kimefanikiwa kuziharibu droni 158 zilizorushwa kutoka Ukraine usiku wa kuamkia leo, zikiwemo tisa zilizoulenga mji wa Moscow na maeneo ya jirani na mji huo.

Hata hivyo Shirika la Habari la Uingereza Reuters halikuweza kuthibitisha taarifa hizo. Na hakujawa na taarifa ya mara moja kuhusu madai ya  mashambulizi hayo kutoka kwa upande wa Ukraine.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW