1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUrusi

Droni za Urusi zadunguliwa na Ukraine

4 Mei 2023

Urusi ilirusha ndege 24 zisizokuwa na marubani usiku wa kuamkia leo dhidi ya Ukraine.

Droni za Urusi zinazoundwa na Iran
Droni za Urusi zinazoundwa na Iran Picha: Aleksandr Gusev/Pacific Press/picture alliance

Hata hivyo Ukraine pamoja na washirika wake, walidungua na kuangusha droni 18 kati ya hizo 24.

Hayo yamesemwa na jeshi la angani la Ukraine lililoeleza zaidi kuwa ndege hizo zilikuwa za Shahed chapa 136/131

Hayo yamejiri siku moja tu baada ya Urusi kuishutumu Ukraine kuhusu jaribio la shambulizi la droni kwenye Ikulu ya Urusi kwa lengo la kutaka kumuua Rais Vladimir Putin

Urusi ilitishia kuchukua hatua kali kama jibu kutokana na madai hayo.

Ukraine imekana kuhusika na shambulizi hilo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW